Stephane Aziz Ki amehitimisha msimu kibabe akifunga hat-trik katika ushindi wa mabao 4-1 ambao Yanga wamepata dhidi ya Tanzania Prisons katika uwanja wa Azam Complex
Ki amekamilisha furaha ya Wananchi baada ya kufikisha mabao 21 akimuacha Feisal Salum wa Azam Fc aliyefunga mabao 19
Azam Fc wamefanikiwa kumaliza nafasi ya pili baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Geita Gold na kuiacha Simba ikimaliza nafasi ya tatu
Yanga na Azam Fc zitacheza ligi ya mabingwa msimu ujao wakati Simba na Coastal Union zikienda Shirikisho
Kwa hakika ulikuwa msmu bora kwa Kocha Miguel Gamondi akivunja rekodi ya Nasreddine Nabi akimaliza msimu na alama 80. Msimu uliopita Nabi alimaliza msimu na alama 78
Kwa Aziz Ki, ni msimu wake bora zaidi katika maisha yake ya kucheza soka akiibuka Mfungaji Bora lakini pia tuzo ya MVP ni yake!