Gamondi avuruga rekodi ya Nabi kwa msimu mmoja

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 May 2024
Gamondi avuruga rekodi ya Nabi kwa msimu mmoja

Msimu wake wa kwanza na Yanga umetosha kudhihirisha Miguel Gamondi ni Kocha wa daraja la juu na kama Wananchi wataendelea kuwa nae kwa muda mrefu pengine atafanya mambo makubwa

Wakati Yanga inamtangaza kuchukua nafasi ya Nasreddine Nabi katik Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Yanga mwaka 2023, hakuna aliyekuwa akimfahamu vyema Kocha huyo zaidi ya Rais wa Yanga Injinia Hersi Said

Lakini msimu wake mmoja umetosha kuwasahaulisha Wananchi kuhusu Nabi ambaye nae anapambana kuipa ubingwa klabu ya FAR Rabat ya Morocco

Katika msimu huu, Gamondi amevuruga rekodi zote za msimu wa mwisho wa mtangulizi wake Nabi

Yanga imemaliza mechi zake 30 msimu huu ikijikusanyia pointi 80, na kuvunja rekodi ya msimu uliopita ilipomaliza ikiwa na pointi 78, hivyo msimu huu imezidi pointi mbili zaidi

Msimu huu, Yanga imemaliza ligi ikishinda michezo 26, hivyo kuvunja rekodi ya msimu uliopita iliposhinda michezo 25, ambapo imezidi mchezo mmoja mbele

Mabingwa hao msimu huu wameongeza idadi ya mabao 10 zaidi ya msimu uliopita, kwani wamepachika mabao 71, wakivunja rekodi ya msimu uliopita, walipomaliza na mabao yao 61, huku pia ikiruhusu idadi ndogo ya mabao ambayo ni 14 tu, wakati msimu uliopita iliruhusu mabao 18, hivyo kuwa pungufu ya mabao manne msimu huu

Rekodi nyingine ya kujivunia kwa Yanga msimu huu ni kushinda mechi zake zote 15 nyumbani, huku ikipata sare mechi tatu ugenini na kupoteza mechi mbili

Kimataifa Yanga imecheza hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kwa mara ya kwanza baada ya kusubiri miaka 25 na zaidi ni kufika robo fainali ya michuano hiyo na kutolewa kwa 'zengwe' nchini Afrika Kusini

Msimu uliopita Nabi aliiwezesha Yanga kucheza fainali ya kombe la Shirikisho na kukosa ubingwa kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya USM Alger

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’