Msimu wa ligi kuu 2023/24 Yanga iliendeleza ubabe wake kwa kutwaa ubingwa kama ilivyofanya katika misimu yote miwili iliyopita
Wananchi wamekusanya jumla ya alama 80, wakishinda mechi 26, wakipoteza mechi mbili na kutoka sare mechi mbili
Katika mechi 26 ambazo Yanga imeshinda, mechi 15 imeshinda nyumbani na mechi 11 ikishinda ugenini, ikitoka sare mara mbili na kupoteza mara mbili ugenini
Yanga imeweka rekodi ya kushinda mechi zote nyumbani katika msimu wa ligi kuu 2023/24
Aidha, Yanga iliweza kuzifunga timu zote 15 zilizoshiriki ligi kuu 2023/24. Ni JKT Tanzania, Azam Fc, Kagera Sugar na Ihefu Fc ambazo zilinusurika kichapo nyumbani na ugenini

ADVERTISE HERE