Klabu ya Yanga leo inafanya Mkutano Mkuu wa mwaka wa Wanachama. Mkutano huo utafanyika Katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano (Julius Nyerere ICC)
Ni utaratibu wa kawaida kwa kila mwisho wa mwaka (msimu) Wanachama ambao kimsingi ndio wamiliki wa klabu kupata taarifa muhimu kuhusu uendeshaji wa klabu yao
Pia kupitia Mkutano huo, Wanachama watafanya tathmini ya Bajeti ya mwaka uliopita na kupitisha Bajeti ya mwaka unaofuata
Mkutano huo unatarajiwa kuanza saa 4 asubuhi na utakuwa 'mbashara' Azam TV
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amewaalika Wanachama katika Mkutano huo huku akiweka bayana kutakuwa na 'surprise'
Je ni usajili mpya au kuna watu muhimu klabuni wameongeza mikataba?
Majibu ya maswali haya yatapatikana wakati Mkutano huo unafungwa...!
ADVERTISE HERE