Mkuchika ataka usajili wa kutisha Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jun 2024
Mkuchika ataka usajili wa kutisha Yanga

Mwenyekiti wa Baraza la wadhamini la Yanga, George Mkuchika ameitaka Kamati ya usajili iwe makini kwenye kufanya usajili wa wachezaji ili waendelee kufanya vema msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Wanachama wa Yanga uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Julius Nyerere jana, Mkuchika alisema baada ya mafanikio ya soka la ndani katika misimu mitatu, sasa kiu yao ni kuona timu inaendelea kufanya vizuri zaidi hasa katika mashindano ya CAF

Mkuchika alisema Wanayanga wanataka kuiona Yanga ikicheza fainali ya ligi ya mabingwa kama walivyofanya katika kombe la Shirikisho msimu wa 2022/23

"Tunataka mfanye usajili wa kutisha ambao utatufanya tuingie hatua ya fainali katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kulibeba Kombe moja kwa moja mpaka kwa Rais Samia"

"Hatupaswi kubweteka kwa mafanikio haya, tufahamu kazi ndio kwanza imeanza, Baraza la Wadhamini tutaendelea kushirikiana na uongozi wa klabu ili kutetea makombe yetu yote msimu ujao," alisema

Aidha Mkuchika aliwataka mashabiki wa Yanga kuendelea kuiunga mkono timu yao kwa kwenda kiwanjani timu hiyo inapocheza

"Tunawaomba mashabiki wa Yanga nanyi msiwe nyuma, hakikisheni mnakwenda uwanjani kujaza uwanja kila timu inapocheza," aliongeza Mkuchika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
3h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
18h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
18h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
22h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’