Licha ya klabu ya Azam Fc kufanya jitihada mshambuliaji Prince Dube asitue kwa Wananchi, jambo hilo limezidi kuwa gumu baada ya Dube kuweka msimamo juu ya timu ambayo atajiunga nayo
Mkataba wa Dube na Azam Fc unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu hata hivyo Azam Fc na Dube walikuwa na makubaliano ya kuongeza mkataba mwingine wa miaka miwili ambapo Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ilithibitisha kuwa Dube alipokea fedha kwa ajili ya kusaini mkataba huo mpya
Dube anatakiwa kurejesha fedha alizopewa na Azam Fc ambapo baada ya kufanya hivyo atakuwa huru kujiunga na timu yoyote
Hata hivyo inavyoonekana ni kuwa Azam Fc ilikuwa tayari kumuachia Dube ajiunge na klabu ya Simba au Al Hilal pasipo kurudisha fedha
Kuna taarifa kuwa jitihada za kumshawishi Dube asaini Simba zimeendelea lakini Dube ameweka ngumu na yuko tayari kutimiza masharti mengine ili aondoke akiwa mchezaji huru
Pengine mwishoni mwa mwezi huu sakata lake na Azam Fc litamalizika na akajiunga na timu ya ndoto zake (Yanga)!