Waziri wa Fedha Mh Dk Mwigulu Nchemba amesema anatamani nembo ya klabu ya Yanga iwekwe katika noti ya Shilingi 100 ili kuyaenzi mafanikio mabingwa hao wa kihistoria
Dk Mwigulu ametoa kauli hiyo Bungeni leo wakati akisoma hotuba ya bajeti kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025
"Yanga ni wafalme wa soka la Tanzania, natamani kumshauri Gavana wa Benki Kuu kuweka nembo ya Yanga kwenye noti ya Shilingi 100 ili kuyaenzi mafanikio haya," alisema Mwigulu ambaye nje ya majukumu yake ya Kiserikali ni Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la Yanga
Aidha Dk Mwigulu alikwenda mbali zaidi akitamani Mfadhili/Mdhamini wa Yanga GSM ajengewe mnara kutokana na uwekezaji aliofanya katika klabu ya Yanga na kuifanya timu hiyo kuwa tishio katika soka la ndani huku ikianza kutamba Kimataifa pia
Yanga ni timu ya kihistoria ambayo ilishiriki katika harakati za ukombozi wa Bara la Afrika
Wananchi wanashilia rekodi ya kutwaa mataji mengi ya ligi kuu na mashindano mbalimbali
Jumamosi, Juni 15, Yanga itazindua kitabu ambacho kitaangazia historia tangu kuundwa kwake mwaka 1935 na mafanikio yake tangu wakati huo