Gamondi afurahia mastaa kubaki Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Jun 2024
Gamondi afurahia mastaa kubaki Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ameeleza kufurahishwa na uongozi wa timu hiyo baada ya kufanikiwa kuwabakisha wachezaji muhimu wa kikosi chake

Baada ya msimu kumalizika, kulikuwa na tetesi nyingi zilizowahusisha baadhi ya wachezaji wa kikosi cha kwanza kuondoka

Gamondi amesema ripoti ya maboresho ya kikosi chake tayari ameikabidhi kwa uongozi wa Yanga lakini jambo lililomfurahisha zaidi ni kuona nyota wake wote muhimu wanaendelea kubaki Jangwani

"Kazi yangu nimeikamilisha, nimekabidhi ripoti haraka ili iweze kufanyiwa kazi hilo nimewaachia viongozi ambao tayari wamenihakikishia kubakiza mastaa wangu wote walionifanyia kazi nzuri msimu ulioisha"

"Endapo wataniongezea na wachezaji wa nafasi nilizopendekeza zifanyiwe kazi basi natarajia kuwa na msimu mwingine bora na naamini wachezaji hawataniangusha kuweza kufikia malengo," alisema Gamondi

Kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki ni miongoni mwa wachezaji ambao tetesi nyingi zilimuhusu hata hivyo Yanga imefanikiwa kumbakisha

Kinachosubiriwa ni taarifa rasmi kutoka kwa uongozi juu ya mfungaji bora huyo msimu uliopita kuongeza mkataba sambamba na nyota wengine ambao mikataba yao imemalizika

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
11h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’