Aliyekuwa winga mahiri wa Yanga, Simon Msuva sasa ataondoka kesho Jumatano kuelekea nchini Morocco kwenda kukamilisha usajili klabu ya Difaa El Jadida.
Msuva alishindwa kuondoka Ijumaa iliyopita baada ya kocha Mkuu wa Stars Salum Mayanga kumtaka nchini Rwanda katika kikosi cha Stars kilichopambana na wenyeji Rwanda katika mchezo wa mtoano wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya CHAN 2018 inayohusisha wachezaji wa ndani itakayofanyika nchini Kenya.
Hata hivyo Stars iliondoshwa kwenye michuano hiyo baada ya kulazimishwa suluhu ya 0-0 huku mchezo wa kwanza uliopigwa jijini Mwanza matokeo yakiwa 1-1.
Msuva ameitengenezea Yanga 'mkwanja' wa kutosha kwani inatarajia kuvuna zaidi ya Mil 300 kwa mauzo yake kama atafuzu vipimo vya afya.
Msuva atafanyiwa vipimo vya Afya na klabu hiyo na kama atafuzu basi atasajiliwa moja kwa moja kuungana na Ramadhani Singano 'Messi' ambaye ameshasajiliwa na klabu hiyo itakayoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao.

ADVERTISE HERE