Dube amepania kuthibitisha ubora wake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jul 2024
Dube amepania kuthibitisha ubora wake

Mshambuliaji wa zamani wa Azam Fc Prince Dube amesema atahakikisha anajipanga ili kuthibitisha ubora wake pale atakapoanza kuitumikia timu yake mpya

Dube kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kutimiza masharti ya kuilipa Azam Fc gharama za mkataba mpya ambao alipaswa kusaini

Dube yuko nchini akisubiri kutambulishwa katika timu yake mpya, Yanga ikitajwa kumalizana na mshambuliaji huyo kutoka Zimbabwe

"Kwanza namshukuru Mungu sana kwa jambo hili kumalizika salama, nilikuwa nasubiri kwa muda mrefu na kwa hamu uamuzi huu. Nawashukuru Azam kwa kukubaliana na ombi langu," Dube alinukuliwa na gazeti la Mwanaspoti

"Ni miezi minne sasa niko nje ya uwanja, ukweli ni kwamba nina hamu sana ya kurudi kucheza soka la ushindani:

"Unapozoea kucheza soka na ikawa tofauti ukiwa huna matatizo yoyote ya afya ilikuwa inaniumiza sana, lakini kwa sasa mambo yamekwisha. Kinachofuata ni kujipanga tu, nataka kujiandaa vizuri ili nitakaporudi nithibitishe uwezo wangu," alisema

Dube aliifungia Azam Fc mabao nane katika msimu uliopita Ligi Kuu ya NBC kabla ya kuikacha timu hiyo mwishoni mwa mwezi Februari

Yanga tayari imempa mkataba wa miaka miwili kinachosubiriwa ni taratibu za utambulisho ambao huenda ukafanyika wiki hii

Dube ataungana na washambuliaji wengine katika kikosi cha Yanga ambao ni Kennedy Musonda na Clement Mzize huku kukiwa na tetesi kuwa Yanga pia imemsajili Jonathan Sowah raia wa Ghana aliyekuwa akiitumikia Al Nasri ya Libya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’