Mwanachama wa Yanga Mzee Juma Magoma amekana taarifa zinazosambaa mtandaoni kuwa yeye pamoja na mwenzake wameshinda kesi dhidi ya Yanga Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu Jijini Dar es salaam katika hukumu iliyotolewa 2023
Akihojiwa na Crown Media mapema leo, Mzee Magoma alisema taarifa hizo ameziona mitandaoni kama watu wengine lakini hana taarifa juu ya ushindi huo anaodaiwa kupata dhidi ya Yanga
"Siwezi kuelewa Mahakama inafanya kazi gani, kwa sababu mimi ndio mstahili wa kupewa hukumu. Hizi ni propaganda. Mimi bado Eng. Hersi ni kiongozi wangu pamoja na bodi yake"
"Lakini kama itatokea jambo lingine lolote kupitia kwangu, mimi mwenyewe nitaita vyombo vya habari nitaongea navyo. Lakini haya yaliyotokea jana (kushinda kesi dhidi ya uongozi Yanga) hakuna ukweli," alisema
Kauli ya Magoma inadhihirisha kuwa yawezekana ni propaganda kwani hata kesi yenyewe inaonekana kufunguliwa mwaka 2022. Kulingana na taarifa iliyosambaa mitandaoni, maamuzi hayo yametoka 2023 August lakini cha kushangaza mjadala umeibuliwa Julai 16 2024 karibu mwaka mmoja tangu hukumu ilipotolewa!