Katika msimu uliopita, Yanga imeongoza kwa kuingiza mashabiki wengi kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara
Huu ni msimu wa nne mfululizo Yanga inaweka rekodi ya kuingiza mashabiki wengi zaidi katika mechi zao, h
Kwa mujibu wa takwimu zilizotokea jana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Yanga imeongoza, ikiingiza jumla ya mashabiki 141,911 kwa msimu, ikifuatiwa na Simba ambayo iliingiza mashabiki 112, 717
Timu ya Mashujaa FC, yenye maskani yake mjini Kigoma, imeshika nafasi ya tatu, ikiingiza mashabiki 45,638, huku Tabora United ikiwa nafasi ya nne, ikikusanya 43,808 na Azam FC, imekuwa ya tano ikiingiza jumla ya mashabiki 35,379.
Kwa mujibu wa takwimu hizo za TFF, nafasi ya sita imechukuliwa na Dodoma Jiji, yenyewe ikiwa na mashabiki 30,381, Geita Gold ambayo imeshuka daraja, ikiwa ya saba, ikiingiza 24,774, Coastal Union ikikamata nafasi ya nane, mashabiki wake ni 24,161, maafande wa Prisons wakiwa kwenye nafasi ya tisa, wakiwa na mashabiki 24,147, na nafasi ya 10 imeenda kwa Singida Fountain Gate, ambayo kwa msimu mzima imeingiza mashabiki 21,154
Mtibwa Sugar ni ya mwisho, ikiingiza mashabiki 7,529, ambayo ndiyo walioingia Uwanja wa Manungu Complex, kutazama mechi za Ligi Kuu msimu uliopita
Hata hivyo Yanga iliathirika katika mapato kwa kuwa mechi 12 kati ya 15 walizocheza nyumbani zilipigwa uwanja wa Azam Complex