Zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya dirisha la CAF la usajili kufungwa, mabingwa wa nchi Yanga ni kama wameshakamilisha usajili wao
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), mpaka sasa Yanga imesajili wachezaji 27 kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa inayotarajwa kuanza kutimua vumbi mwezi ujao
Msemaji wa Yanga Ali Kamwe nae amethibitisha kuwa usajili wa Kimataifa umekwenda vizuri japo kuna wachezaji bado hawajatambulishwa kutokana na sababu mbalimbali
"Usajili wetu kwa ajili ya Ligi ya Mabingwa umekwenda vizuri japo kuna wachezaji hatujawatambulisha. Kuna mambo tunaweka sawa lakini ndani ya siku hizi mbili kila kitu kitawekwa hadharani," alisema Kamwe
ADVERTISE HERE