Maxi ameanza na gia kubwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Jul 2024
Maxi ameanza na gia kubwa

Kwa aina ya maboresho ya kikosi ambayo Yanga wamefanya katika dirisha hili la usajili, Wananchi watarajie kuona ushindani mkali katika kikosi cha kwanza

Lakini ushindani huo unaweza usihusishe eneo ambalo anacheza Maxi Nzengeli kwani anaonekana msimu huu amerejea akiwa na ari ileile

Juzi katika mchezo wa ufunguzi wa Mpumalanga Premier's International Cup dhidi ya Ausburg, Maxi ni mchezaji pekee ambaye hakufanyiwa mabadiliko katika safu ya ushambuliaji

Wachambuzi wanasema tank la mafuta la Maxi limejaa muda wote, pengine ndio sababu katika mchezo huo aliwahenyesha kwelikweli Wajerumani

Bao pekee la Yanga lililofunga na Jean Baleke lilitokana na krosi ya Maxi ambaye pia alimanusra aifungie Yanga katika kipindi cha kwanza kama sio shuti lake kugonga mwamba

Baada ya mchezo Wajerumani walimfuata Maxi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kumpongeza na kuomba kubadilishana jezi

Kwa hakika Rais wa Yanga Injinia Hersi Said anapaswa kuanza mapema mazungumzo ya kumuongeza mkataba ili kuhakikisha anaendelea kuwa mali ya Wananchi kwa miaka mingi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’