Kamwe adokeza mpinzani wa Yanga Wiki ya Mwananchi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jul 2024
Kamwe adokeza mpinzani wa Yanga Wiki ya Mwananchi

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema wako kwenye mazungumzo ya mwisho na timu watakayochuana nayo katika mchezo wa kilele cha Wiki ya Mwananchi ambao utapigwa August 04 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Kamwe amesema awali walikuwa wakifkiri kuleta timu kutoka barani Ulaya lakini sasa wamesitisha mpango huo baada ya kupata timu yenye sifa wanazohitaji hapa barani Afrika

"Unajua tulizialika timu kadhaa kubwa lakini wengi wamehofia kukutana nasi isipokuwa huyu mmoja ambaye tunakamilisha nae maungumzo"

"Ni timu kubwa ambayo imewahi kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa, hawa watakuja kwa Mkapa tuonyeshane kazi August 04"

"Msimu huu tumeweka malengo makubwa, tunataka ubingwa wa Afrika, ndio maana unaona hata maandalizi yetu ni tofauti, tunacheza na timu kubwa tu"

"Mechi zetu sisi wapinzani wanafahamika, na hatuchezi gizani kama timu nyingine," Kamwe aliwatupia dongo watani zake Simba

Kabla ya kurejea nchini kwa ajili ya Wiki ya Mwananchi, Yanga itacheza mechi mbili Afrika Kusini

Kesho Jumatano wataumana na TS Galaxy mchezo ambao utarushwa mbashara na Azam TV na kuhitimisha mchezo wa mwisho Jumapili Julai 28 dhidi ya Kaizer Chiefs katika Toyota Cup

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
3h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
3h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
7h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
22h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’