Ngao ya Jamii hakuna extra-time

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 Jul 2024
Ngao ya Jamii hakuna extra-time

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB), imebainisha kuwa hakutokuwa na dakika za nyongeza kwa michezo yote itakayopigwa kwenye Ngao ya Jamii inayotarajiwa kuanza kupigwa Agosti 8, mwaka huu

Ofisa Habari wa Bodi hiyo, Karim Boimanda, amesema mechi zote zitachezwa kwa dakika 90 na baada ya hapo ni mikwaju ya penalti itaamua mshindi

Boimanda alisema hayo, alipokuwa akibainisha baadhi ya kanuni zitakazotumika kwenye michuano hiyo, pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara inayotarajiwa kuanza Agosti 16, mwaka huu

Mbali na hayo, amesema wachezaji watakaotumika kwenye mechi hizo ni wale tu ambayo watakuwa wamekamilisha usajili wa kucheza Ligi Kuu na si vinginevyo kwani huko nyuma imeshawahi kutokea timu moja kuchezesha kwenye Ngao ya Jamii mchezaji ambaye baadaye ilibainika bado alikuwa hajakamilisha taratibu za kucheza ligi

"Wachezaji wanaoruhusiwa kucheza Ngao ya Jamii ni wale ambao usajili wao umekamilika tu, ambao wameshasajiliwa kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa na hakutokuwa na dakika za nyongeza kwa mechi zote, kuanzia za nusu fainali, fainali hadi kusaka mshindi wa tatu, zikiisha dakika 90, zitapigiana mikwaju ya penalti," alisema Ofisa Habari huyo

Kanuni nyingine ni kwamba, mchezaji yeyote ambaye alimaliza Ligi Kuu msimu uliopita akiwa na kadi nyekundu au adhabu ya kusimamishwa hata mechi moja kwa kuwa na kadi tatu za njano na hakuzitumikia kwa sababu ligi ilikuwa imemalizika, hatoruhusiwa kucheza kwani atatakiwa kutumikia adhabu yake

"Kanuni hizi zinatumika pia kwenye Ligi Kuu. Kwa hiyo hata adhabu zinaingiliana, mchezaji mwenye kadi na hakutumikia hatatusubiri mpaka ligi hivyo atazitumikia kwenye Ngao ya Jamii. Lakini yeyote ambaye atapata kadi nyekundu kwenye michezo hiyo, ataitumikia pia kwenye michezo ya ligi," alisema

Alisema wameamua kuanika baadhi ya kanuni hizo kutokana na mashabiki wengi kuwa na mkanganyiko hasa inapokuwa michezo kama hiyo ambayo ni ya mtoano, wasijue nini kinafuata baada ya timu kutoka suluhu

Agosti 8, saa 10:00 jioni, Azam itakipiga dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Na saa 1:00 usiku Simba itavaana na Yanga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam na fainali ya Ngao ya Jamii itapigwa hapohapo Agosti 11, mwaka huu

IPP Media

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
34m ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
58m ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
4h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
19h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
23h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’