Yanga imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya TS Galaxy katika mchezo wa pili wa Mpumalanga Premier's International Cup
Prince Dube 'Mwana Mfalme' ndiye aliyefunga bao pekee la Yanga katika kipindi cha pili baada ya pasi kutoka kwa Aziz Ki
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi alitumia vikosi viwili ambapo kipindi cha kwanza alianza na timu nyingine na kubadili kikosi kizima katika kipindi cha pili
Nyota wengi wa kikosi cha kwanza waliingia katika kipindi cha pili na walionyesha utofauti mkubwa wa kiuchezaji na pengine wangefunga mabao zaidi
Ulikuwa mchezo wa maandalizi mazuri kwa Yanga kuelea mchezo dhidi ya Kaizer Chiefs siku ya Jumapili
ADVERTISE HERE