Khalid Aucho amecheza dakika 45 za mchezo dhidi ya TS Galaxy leo akiwa katika ubora mkubwa kana kwamba amefanya mazoezi muda mrefu na timu
Ni wazi Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi atakuwa na mtihani wa kuamua wachezaji atakaowatumia katika kikosi chake cha kwanza kwani kila mmoja anataka namba
Aziz Andambwile leo katumika kama beki wa kati, kama humfahamu unaweza kudhani amekuwa akicheza katika nafasi hiyo kwa muda mrefu
Pata picha Andambwile arudishwe eneo la kiungo cha chini acheze pacha na Aucho halafu mbele yao wacheze Chama/Pacome/Abuya, Aziz Ki na Maxi Nzengeli huku eneo la ushambuliaji wapo Prince Dube, Jean Baleke, Kennedy Musonda na Clement Mzize
Kwa hii Yanga ya msimu huu kuna watakaogoma kuleta timu uwanjani...!
Gamondi na benchi lake la ufundi nao kazini kwao kuna kazi kwani kila mchezaji anaitaka namba katika kikosi cha kwanza