Aziz Ki anastahili tuzo tatu - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jul 2024
Aziz Ki anastahili tuzo tatu - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema kiungo mshambuliaji wa Yanga Stephane Aziz Ki ambaye ni mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC msimu uliopita, anastahili kubeba tuzo ya mchezaji bora wa msimu (MVP) lakini pia anastahili kubeba tuzo ya kiungo bora

Kamwe amesema itakuwa jambo la kushangaza kama Aziz Ki hatashinda tuzo ya kiungo bora kwa kuwa ndiye kiungo aliyekuwa na takwimu nzuri zaidi msimu uliopita (ku-assit na kufunga)

Aziz Ki anawania tuzo ya MVP na kiungo bora ambapo katika kinyan'ganyiro hicho yumo Feisal Salum aliyefunga mabao 19 akishika nafasi ya pili nyuma ya Ki aliyebuka mfungaji bora na mabao 21

Aziz Ki pia alitoa assist nane moja zaidi ya Feisal ambaye alitoa assist saba wakati Kipre Junior wa Azam Fc akitoa assist 9 na kuongoza

Hata hivyo ni Aziz alikuwa na takwimu bora za jumla (magoli na assist) kuliko Feisal na Kipre anaochuana nao katika tuzo hiyo

"Kama mnakubali MVP atatokea kwenye nafasi ya kiungo, na akaweza kufunga Magoli mengi zaidi (Top Scorer kwa Goli 21), akiziwa Asisti MOJA TU na winga, itakuwa ni habari ya kushtua zaidi duniani kama mchezaji huyo hatapewa pia TUZO YA KIUNGO BORA WA MSIMU"

"Hili halipaswi kabisa kuwa sehemu ya Mjadala. FACTS na NAMBA Ziachwe zizungumze zenyewe. Ingeweza kuwa hoja kama kiungo mmoja anacheza chini (Eneo la ukabaji) na mwingine anacheza Juu (Eneo la kushambulia), lakini kama wote role yao ilikuwa moja uwanjani"

"HAKUNA NAMNA nyingine ya kupindisha pindisha maneno kama mchezaji anacheza eneo la kiungo wa juu jukumu lako la msingi uwanjani ni kutengeneza nafasi na kufunga inapobidi. Katika Ligi Kuu ya NBC, msimu uliopit Aziz Ki KAFANYA VYOTE KWA UBORA MKUBWA MNO," aliandika Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
12h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’