Kesho Yanga itakamilisha mchezo wa Toyota Cup dhidi ya Kaizer Chiefs ambao utapigwa uwanja wa Toyota, Bloemfontein huko Afrika Kusini
Baada ya mchezo huo kikosi cha Yanga kitarejea jiijini Dar es salaam kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea Wiki ya Mwananchi ambayo kilele chake ni August 04 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Lakini bado Wananchi wanahoji wanakwendaji kwenye wiki ya Mwananchi wakati jezi mpya bado?
Habari njema ni kuwa Yanga iko tayari kuzindua jezi mpya za 2024/25 ambapo ni suala la muda tu, Yanga imethibitisha jezi hizo zitazinduliwa leo
Mbunifu wa jezi za Yanga Sheria Ngowi ametamba kuwa anakwenda kufunika kelele zote na kudhihirisha kuwa amewaacha mbali sanaaaa
ADVERTISE HERE