Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amebeba tuzo ya Kocha bora wa Ligi Kuu ya NBC, 2023/24
Gamondi amestahili kushinda tuzo hiyo baada ya kuingoza Yanga kutwaa taji la Ligi kuu ikikusanya alama 80 na pia akiwaongoza Wananchi kushinda taji la Shirikisho la CRDB
Aidha mshambuliaji Clement Mzize ametwaa tuzo ya mfungaji bora kombe la CRDB huku Djigui Diarra akishinda tuzo ya kipa bora wa michuano hiyo
Stephane Aziz Ki ndiye mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC pia akibeba tuzo ya kiungo bora. Ki pia anatarajiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu MVP
Meneja wa habari wa Yanga Ali Kamwe alipokea tuzo kwa niaba ya Mzize
ADVERTISE HERE