Diarra ataendelea kuwaimarisha Mshery, Khomein

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Aug 2024
Diarra ataendelea kuwaimarisha Mshery, Khomein

Makipa wa Yanga, Abuutwalib Mshery na Khomein Abubakar wataendelea 'kuchota madini' kwa mlinda lango namba moja wa Yanga Djigui Diarra ambaye bado yuko mikononi mwa Wananchi kwa misimu mingine mitatu baada ya kuongeza mkataba

Diarra aliyesajiliwa na Yanga Agosti 2021 akitokea Stade Malien ya Mali mkataba wa sasa na Yanga ulikuwa unatamatika mwisho wa msimu wa 2024/25, hivyo Kwa kusaini mkataba mpya wa miaka miwili unamuweka Diarra Jangwani mpaka msimu wa 2026/27

Diarra tangu ametua kwa Wananchi amefanikiwa kuibuka kipa bora wa msimu mara mbili mfululizo na ameisaidia timu hiyo kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu Bara mfululizo na mataji matatu ya Kombe la Shirikisho (FA)

Juzi katika kilele cha Wiki ya Mwananchi, Rais wa Yanga Injinia Hersi Said alipewa jukumu la kutambulisha mchezaji mmoja ambapo akamtambulisha Diarra huku akifichua kuwa amesaini mkataba mpya utakaomuweka Jangwani hadi mwaka 2027

Uwepo wake utaendelea kuwapa nafasi ya kujifunza na kuimarika zaidi walinda lango wazawa Mshery n Khomein aliyesajiliwa katika dirisha hili akitokea klabu ya Singida Black Stars

Diarra kwa sasa ndio kipa namba moja wa timu ya Taifa ya Mali ambapo mapema mwaka huu katika michuano ya Afcon 2024 iliyofanyika Ivory Coast, Diarra aliisaidia Mali kufika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo huku akiwa mlinda lango namba moja

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
20m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’