Yanga imetinga fainali ya Ngao ya Jamii baada ya kuichapa Simba bao 1-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Aliyepeleka kilio Msimbazi ni yuleyule Maxi Nzengeli katika dakika ya 44 akilitendea haki shambulizi lililofanywa na Yanga baada ya Aucho, Pacome, Maxi mwenyewe na Prince Dube kupigiana pasi
Ulikuwa mchezo mzuri ambapo Yanga ilitawala zaidi kipindi cha kwanza na pengine ilistahili kufunga mabao zaidi Prince Dube akigongesha mwamba mapema katika kipindi cha kwanza
Mechi ilikuwa nzuri Simba wakitoa upinzania hasa katika kipindi cha pili lakini Yanga imeendelea kudhihirisha bado ndio wafalme wa mechi za dabi kwa sasa
Huo ni ushindi ws tatu mfululizo Yanga inapata ushindi dhidi ya Simba, ikifunga jumla ya mabao nane na kuruhusu mabao mawili tu