Kwa pasi za Chama nitafunga sana magoli - Mzize

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Aug 2024
Kwa pasi za Chama nitafunga sana magoli - Mzize

Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize amesema ubora wa pasi ya mwisho ya Clatous Chama ulimpa urahisi kuifungia Yanga bao la nne katika mchezo wa fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam Fc uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa juzi

Mzize alifunga bao la nne na la mwisho kwenye ushindi wa mabao 4-1 ilioupata Yanga dhidi ya Azam katika fainali ya Ngao ya Jamii iliyochezwa juzi Jumapili kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam. Mabao mengine yalifungwa na Prince Dube, Yoro Diaby (alijifunga) na Stephane Aziz Ki. Bao la Azam lilifungwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Mzize amefichua kuwa kabla ya kuingia uwanjani akitokea benchi, Kocha Miguel Gamondi alimtaka kuhakikisha anatumia nguvu zote kupeleka mashambulizi kwa wapinzani na ndicho alichokifanya

"Alinionyesha mianya mingi ya kupita na kunisisitiza kutumia nguvu na akili kusogeza mashambulizi kwa wapinzani ndicho nilichokifanya, bao nililofunga nilianza kulitengeneza mwenyewe kwa kukokota mpita kutoka eneo la mbali la uwanja," alisema na kuongeza;

"Baada ya kusogea karibu na boksi nilimpa pasi Chama ambaye ana jicho zuri la kutoa pasi za mwisho na kuwahi kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kupachika bao bila hiyana kiungo fundi wa pasi za mwisho alitoa pasi kwenye nafasi nzuri na mimi nilikwamisha mpira kambani"

Mzize alisema Chama ni mchezaji ambaye anapiga pasi za akili na bora hivyo akiwa katika mazingira ambayo hakutarajia alikutana na mpira mguuni na kuukwamisha nyavuni.

"Chama ana jicho la kutoa pasi za mwisho na endapo kila mchezaji atacheza naye kwa usahihi basi atatulisha sana mipira ya mwisho na tutafunga sana, hili ni trela picha kamili linakuja," alitamba Mzize.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
2h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
13h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
20h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’