Tumeongeza wachezaji bora - Hersi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
16 Aug 2024
Tumeongeza wachezaji bora - Hersi

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema anaamini nyota wapya waliosajiliwa katika dirisha la usajili lililofungwa jana watakuwa na mchango mkubwa msimu huu

Hersi amesema anaamini uzoefu na ubora wa wachezaji kama Clatous Chama, Prince Dube, Duke Abuya, Chadrack Boka na wengine utakuwa na faida kubwa kwa timu hiyo

Aidha Hersi amewapa ujumbe wale wanaodai Chama amezeeka, wasubiri kuona mchango wake katika kikosi cha Yanga msimu huu

"Chama ni moja ya wachezaji bora waliofanya vyema katika ligi kuu ya Tanzania Bara misimu ya karibuni. Huyu ni mchezaji wa daraja la juu isiwe kwa kuwa Yanga imemsajili aonekane ni mchezaji wa kawaida"

"Nikwambie tu, haikuwa rahisi kumsajili Chama kwani hata huko alikotoka hawakuwa tayari kuona anaondoka. Chama ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa, tusubiri mwisho wa msimu halafu utauona mchango wa Chama kwa Yanga," Hersi aliiambia BBC Swahili

Aidha Hersi pia amesema mshambuliaji Prince Dube ameanza vyema majukumu yake katika kikosi cha Yanga na ana imani msimu huu atafunga zaidi ya mabao 20

"Mpaka sasa katika mechi hizi tulizocheza Dube amehusika katika mabao zaidi ya matano, akiwa amefunga mabao matatu. Huyu ni mshambuliaji hatari ambaye ana umahiri wa kipekee katika kufunga mabao"

"Kwa jinsi timu yetu inavyocheza na kutengeneza nafasi, kama Dube atafunga chini ya mabao 20 msimu huu basi atakuwa amefeli," aliongeza Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’