Michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika imerejea ambapo leo mabingwa wa nchi Yanga wako uwanjani kumenyana na Vital'o ya Burundi
Ni katika uwanja wa Azam Complex ndipo mchezo huo unatarajiwa kupigwa, saa 10 jioni
Yanga watakuwa wageni katika mchezo ambao Wananchi wanahitaji kushinda ili kurahisisha kazi kwenye mchezo wa marudiano ambao utapigwa Jumamosi ijayo katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Vital'o wako nchini kwa takribani wiki nzima na kelele zao zimekuwa nyingi katika vyombo vya habari
Wanasema usiku wa deni hauchelewi kucha! Hatimaye siku yenyewe imefika, majibu yatapatikana Azam Complex kuanzia saa 10 jioni
Baada ya kutwaa Ngao ya Jamii kwa kuifumua Azam Fc mabao 4-1, Yanga imepata wakati mzuri wa kujiandaa na mchezo huo
Matarajio ya mashabiki wa Yanga ni kuona timu yao ikiibuka na ushindi mnono jioni ya leo
Kila la kheri Wananchi...!