Gamondi awaonya Vital'o

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
18 Aug 2024
Gamondi awaonya Vital'o

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema vijana wake wamewaonyesha Vital'o ukubwa wao na anaamini siku nyingine watakapokuja kucheza na Yanga wataweka heshima mbele

Gamondi alikerwa na kauli zilizotolewa na msemaji wa Vital'o Fc Arsene Bucuti katika mikutano yake na wanahabari kuelekea mchezo huo

Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo huo wa mkondo wa kwanza hatua ya awali ya ligi ya mabingwa, ambapo kocha Gamondi amesema bado hawajamaliza, wanawasubiri tena uwanja wa Benjamin Mkapa kumalizana nao

"Vital'o walizungumza sana kabla ya mchezo, nafikiri ni muhimu kumuheshimu mpinzani wako. Tumewaonyesha sisi ni timu kubwa, mabingwa wa Tanzania. Mimi sikuwafahamu Vital'o kabla ya kukutana nao leo"

"Wachezaji wangu walicheza kwa ari na morali kubwa na niwaambie tu, katika mchezo wa marudiano uwanja wa Benjamin Mkapa tutacheza kwa nguvu zaidi kuliko mechi hii," alisema Gamondi

Baada ya mchezo Gamondi alionekana kuzungumza na msemaji wa Vital'o ambaye kitu pekee anachoweza kujivunia ni kupata umaarufu kutokana na 'mikwara' aliyotoa kabla ya mechi lakini ndani ya dimba, Vital'o hawakuwa na ubavu wa kushindana na Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
1h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
5h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
10h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
13h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’