Mapema tu mshambuliaji Prince Dube ameingia katika mfumo wa Kocha Miguel Gamondi akiwa chaguo la kwanza la Muargentina huyo
Wakati Yanga inamsajili mshambuliaji huyo yalisemwa mengi kuwa ameisha na ni mchezaji ambaye majeruhi hayatamuacha salama
Lakini mpaka sasa Yanga tayari imeanza kunufaika na usajili huo. Katika mechi saba alizoitumikia Yanga, Dube amepachika mabao manne na kutoa assist mbili
Amehusika kwenye mabao sita, pengine ndiye mchezaji aliyehusika kwenye mabao mengi zaidi katika kikosi cha Yanga ndani ya mwanzo huu wa msimu
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema ana matumaini makubwa nyota huyo raia wa Zimbabwe, msimu huu atafunga zaidi ya mabao 20 katika mashindano yote
"Kama Dube hatafikisha mabao 20 msimu huu kwangu mimi atakuwa amefeli kwani mpaka sasa amefikia matarajio ya usajili wake Yanga," alisema Hersi katika moja ya mahojiano aliyofanya hivi karibuni