Jumamosi August 24 Yanga itakuwa uwanja wa Benjamin Mkapa kumalizana na Vital'o katika mchezo wa mkondo wa pil hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika
Hii ni Jumamosi ya burudani kwa mashabiki wa Yanga kwani mchezo huu utatumika kama uzinduzi rasmi wa michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu
Katika Mkutano na Wanahabari jana, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe alisema wamepanga kutumia mchezo huu kuonyesha dhamira yao katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu
Yanga imejiwekea malengo makubwa ambapo Wananchi wanataka kuvuka hatua ya robo fainali ambayo waliishia msimu uliopita
Mashabiki wa Yanga wameaswa kununua tiketi zao mapema ili kujaza dimba la Benjamin Mkapa ili kuionyesha Afrika ukubwa wao
ADVERTISE HERE