Maxi Nzengeli ameanza msimu huu kwa kasi kubwa akiendeleza pale alipoishia msimu uliopita
Katika mechi chache kuanzia kwenye pre-season Afrika Kusini na Ngao ya Jamii, ni wazi Maxi ndiye mchezaji aliyetumika kwa dakika nyingi kuliko wengine
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amekuwa akifanya mabadiliko katika eneo la kiungo lakini si kwa eneo analocheza Maxi
Maxi na Khalid Aucho wamejitengenezea ufalme katika eneo hilo huku Mudathir Yahya sasa akipata ushindani kutoka kwa Duke Abuya
Katika msimu huu Wananchi watarajie makubwa zaidi kutoka kwa kiraka huyo ambaye Kaizer Chiefs walijaribu kumsajili wakati Yanga ilipokuwa Afrika Kusini
Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amehakikisha Maxi na nyota wengine muhimu wanaendelea kubaki kikosini
Msimu huu Yanga imepania kufanya vizuri zaidi katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
