Matchday : Yanga vs Vital'o, CAF CL R2

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Aug 2024
Matchday : Yanga vs Vital'o, CAF CL R2

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga leo wanashuka uwanja wa Azam Complex, saa 1 usiku kuikabili Vital'o kutoka Burundi ukiwa ni mchezo wa mkondo wa pili kuwania tiketi ya kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika

Yanga itashuka Azam Complex leo ikiwa inaongoza kwa mabao 4-0, ushindi waliopata katika mchezo wa kwanza

Leo wananchi watahitaji ushindi au hata sare ili kusonga mbele hatua inayofuata

Vital'o watakuwa na mlima mrefu zaidi kwani ili waweze kufuzu watahitaji kuifunga Yanga mabao 5-0, ni muujiza tu ambao unaweza kufanya matokeo haya yatokee ingawa upo msemo kuwa hakuna lisilowezekana katika mpira wa miguu

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema licha ya ushindi mnono katika mchezo wa kwanza, hatawadharau wapinzani wake na watapambana ili kuhakikisha wanapata matokeo muhimu ili wafuzu hatua inayofuata

Yanga itautumia mchezo huo kuzindua msimu mpya wa michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika 2024/25 ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
43m ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
12h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
16h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
20h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
21h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’