Yanga imefuzu raundi ya kwanza ligi ya mabingwa kibabe baada ya kuifumua Vital'o mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex
Ni ushindi wa jumla wa mabao 10-0 ambao Yanga wameandikisha baada ya ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa kwanza
Leo ilikuwa mechi ya kukusanya fedha kupitia goli la Mama, ambapo Milioni 30 zimepatikana kupitia ushindi huo
Hata hivyo mabao sita pengine yalikuwa machache kwa kuzingatia idadi ya nafasi ambazo Yanga walitengeneza
Vital'o walimaliza 9 uwanjani baada ya wachezaji wawili kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kutumia mikono yao badala ya miguu...!
Clatous Chama alikuwa shujaa wa Yanga katika mchezo huo akifunga bao moja na kutoa assist nne kwa mabao ya Clement Mzize, Aziz Ki, Prince Dube na Mudathir Yahya
Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Pacome Zouzoua kupitia mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Vital'o kuokoa kwa mikono shuti la Pacome lililokuwa linaelekea kimiani
Yanga sasa inafuzu raundi ya kwanza na katika hatua hiyo itachuana na CBE ya Ethiopia ambayo iliitoa SC Villa ya Uganda