Yanga ruksa kutumia New Amaan Complex CAF CL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Aug 2024
Yanga ruksa kutumia New Amaan Complex CAF CL

Yanga imedhamiria kucheza mechi ya mkondo wa pili raundi ya kwanza michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya CBE katika uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar

Uwanja wa New Amaan Complex umeidhinishwa na CAF kutumika kwa ajili ya mechi za Kimataifa ikiwa ni pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Msemaji wa ZFF Spesho Kabwanga amesema uwanja huo awali ulizuiwa kwa kuwa haukukidhi baadhi ya vigezo vya CAF lakini baada ya kufanyiwa marekebisho muhimu, uwanja huo umeruhusiwa kutumika

"Uwanja wa New Amaan Complex umekidhi vigezo vya CAF na tayari umepata ruksa ya kutumika katika mechi za Kimataifa. Kuna vigezo na masharti ambayo CAF walitupatia kuhakikisha tunakidhi kabla ya uwanja kupitishwa"

"Tulifanya marekebisho na kuzingatia vigezo walivyotupatia na tukawatumia uthibitisho wa kila maboresho yaliyofanyika na sasa uwanja tayari umeruhusiwa kutumika," alisema Kabwanga

Kabwanga ametoa ufafanuzi huo na kukanusha taarifa zinazoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa uwanja huo haujakidhi vigezo vya CAF na ndio sababu hauko miongoni mwa orodha ya viwanja vilivyoidhinishwa na CAF kutumika katika michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho msimu huu

Yanga itachuana na CBE ya Ethiopia katika mechi za raundi ya kwanza kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya CAF CL

Mchezo wa kwanza utapigwa Ethiopia katika dimba la Abebe Bikila Septemba 13-15 na marudiano kupigwa Tanzania Septemba 20-22

Huenda mechi hiyo ya marudiano ikapigwa uwanja wa New Amaan Complex..

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
9h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’