Mshambuliaji wa Yanga Clement Mzize ameendelea kuonyesha sababu kwa nini timu nyingi zimepiga hodi Jangwani kuitaka huduma yake
Msimu huu Mzize ameuanza akiwa katika kiwango bora na pengine unaweza kuwa msimu ambao anaweza kuandikisha mafanikio makubwa
Akitokea benchi jana katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar, Mzize aliifungia Yanga bao la pili na kuwahakikishia Wananchi ushindi wa mabao 2-0 ugenini ukiwa ni ushindi wa kwanza msimu huu
Mzize amefunga katika mechi nne mfululizo ambazo zote alitokea benchi. Alipachika bao dhidi ya Azam Fc pia akafunga katika mechi zote mbili za hatua ya awali ligi ya mabingwa dhidi ya Vital'o ya Burundi
Licha ya presha kubwa kutoka klabu mbalimbali ndani na nje ya Afrika, uongozi wa Yanga umeweka msimamo wa kutomuuza Mzize ambapo kama kuna ulazima kwa mchezaji huyo kuondoka basi timu inayomuhitaji itapaswa kufuata masharti ya mkataba wake ambapo italazimika kulipa takribani Tsh Bilioni 2.7
Wydad Athletic walipandisha ofa yao ambayo kwa kuzingatia makubaliano, ingeweza kufikia Bil 1.8 lakini Wananchi wamesema HAPANA