Gamondi akosoa ratiba Ligi ya Mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Aug 2024
Gamondi akosoa ratiba Ligi ya Mabingwa

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amekosoa utaratibu wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) katika ratiba ya mashindano ya CAF ngazi ya klabu na timu za Taifa

Kwa sasa ligi mbalimbali zimesimama Afrika ili kupisha ratiba ya kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2025 kwa timu za Taifa na punde itafuatiwa na ratiba ya CAF kwa klabu

Utaratibu huu umekuwa ukiziumiza klabu zinazoshiriki michuano ya CAF hasa zile zinazotoa wachezaji wengi katika timu za Taifa

"Mimi sikubaliani na utaratibu huu wa ratiba za mashindano ya CAF (klabu na timu za Taifa) kufuatana kwa ukaribu"

"Mfano sisi Yanga tunapaswa kucheza Septemba 13 Ethiopia wakati mechi za timu za Taifa zitahitimishwa Septemba 10, kwa wachezaji wetu ambao wanakwenda timu za Taifa maana yake hawatakuwa na muda wa mapumziko kwa sababu wakitoka timu za Taifa pengine watalazimika kusafiri moja kwa moja kuelekea Ethiopia"

"Tuna wachezaji 14 ambao wameitwa timu za Taifa hivyo, ni ratiba ambayo inasababisha changamoto kwa klabu kwa sababu wachezaji watalazimika kusafiri muda mrefu," alisema Gamondi

Mazingira kama haya yalitokea kwa Yanga msimu uliopita wakati ilipokwenda Algeria kucheza mechi ya kwanza ya hatua ya makundi ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouizdad na kupoteza mchezo kwa kufungwa mabao 3-0

Katika mchezo huo mlinda lango Djiguo Diarra alishindwa kuungana na timu Algeria baada ya changamoto ya kusafiri pale alipomaliza majukumu ya timu ya Taifa huku Stephane Aziz Ki akitua Algeria usiku wa kuamkia siku ya mchezo

Yanga ina wachezaji 14 ambao wako kwenye majukumu ya timu za Taifa na pengine baadhi yao watalazimika kusafiri moja kwa  moja Ethiopia baada ya mechi za timu za Taifa kukamilika

Djigui Diarra, Aboutwalib Mshery, Nickson Kibabage, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Bakari Nondo Mwamnyeto na Mudathir Yahya

Wengine ni Khalid Aucho, Duke Abuya, Stephane Aziz Ki, Clatous Chama, Kennedy Musonda, Prince Dube na Clement Mzize

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
12h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
15h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
20h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
21h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’