Yanga hii wengi watashangilia kufungwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Aug 2024
Yanga hii wengi watashangilia kufungwa

Juzi baada ya mchezo kati ya Kagera Sugar dhidi ya Yanga, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Paul Nkata aliweka bayana kuwa kufungwa mabao 2-0 na Yanga ni kama ushindi kwao kwani wamecheza dhidi ya timu bora zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na kati

Nkata alikwenda mbali zaidi kwa kusema Yanga imezifunga timu kubwa mabao manne na nyingine matano huku akitolea mfano klabu ya Vital'o iliyobugizwa jumla ya mabao 10-0 katika mechi mbili za hatua ya awali ligi ya mabingwa barani Afrika

Kauli ya Nkata imeonyesha uhalisia wa daraja ambalo Yanga imejiweka dhidi ya timu nyingine. Inapotokea timu pinzani inashangilia kufungwa mabao machache hiyo inakuonyesha utofauti wa daraja la ubora

Hata mchezo wa nusu fainali ya Ngao ya Jamii ambao Simba walifungwa bao 1-0 na Yanga, mashabiki wa timu hiyo hawakuchukizwa na kipigo hicho zaidi walitamba kuwa timu yao imeimarika

Matarajio ya wengi katika mchezo huo ilikuwa Simba kuoga mvua ya mabao na ingekuwa hivyo kweli kama sio makosa ya kibinadamu ya waamuzi!

Itoshe kusema Yanga wana ligi ya peke yao, wengi watashangilia kufungwa msimu huu

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
7h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
11h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
16h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’