Wachezaji 7 wa Yanga ambao wako katika kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', leo watakuwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kuiwakilisha nchi kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2025 dhidi ya Ethiopia
Mlinda lango Aboutwalib Mshery, walinzi Nickson Kibabage, Dickson Job, Ibrahim Bacca, Bakari Mwamnyeto kiungo Mudathir Yahya na mshambuliaji Clement Mzize wamejumuishwa katika kikosi cha Stars. Mechi ya pili ya Stars itakuwa ugenini dhidi ya Guinea, Septemba 10
Prince Dube yeye atakuwa dimbani Septemba 06 akiiwakilisha Zimbabwe dhidi ya nyota mwenzake wa Yanga, Duke Abuya anayeitumikia timu ya Taifa ya Kenya
Septemba 06 pia, Daktari wa mpira Khalid Aucho atakuwa Afrika Kusini kupeperusha bendera ya Uganda dhidi ya wajukuu wa Nelson Mandela
Stephane Aziz Ki yeye atakuwa na Burkina Faso kuikabili Senegal Septemba 06 wakati Djigui Diarra atakuwa nyumbani Mali kuiwakilisha nchi yake katika mchezo dhidi ya Msumbiji
Nyota wengine wa Yanga Kennedy Musonda na Clatous Chama wao watakuwa ugenini Ivory Coast kuiwakilisha Zambia
Wachezaji 14 wa Yanga watamaliza majukumu ya kuzitumikia timu za Taifa Septemba 10