Yanga Princess unyonge sasa basi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Sep 2024
Yanga Princess unyonge sasa basi

Wanasema kimya kingi kina mshindi mkuu! Ndivyo unavyoweza kusema kwa kile kinachoendelea katika kikosi ya Yanga Princess

Uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said msimu huu wameweka nguvu kubwa katika kikosi cha Yanga Princess ili kuhakikisha timu hiyo inamaliza unyonge katika ligi kuu ya Wanawake

Aina ya usajili uliofanyika, maandalizi yanayoendelea uwanja wa KMC ni dalili njema kuwa msimu huu kazi ipo ligi ya Wanawake

Yanga Princess imeshusha nyota kadhaa kutoka nje wakiwemo mlinda lango wa timu ya Taifa ya Nigeria Rita Akarekor pamoja na kiungo Toluwalashe Adeshola ambaye alikuwa MVP ligi ya Wanawake Nigeria msimu uliopita

Danai Bhobho kiungo wa Kimataifa wa Zimbabwe ambaye msimu uliopita aliitumikia Simba Queens nae amejiunga na Yanga Princess

Kocha Mkuu wa Yanga Princess Edna Lema amesema wameunda timu mpya ambayo anaamini msimu huu itarejesha heshima ya Yanga upande wa ligi ya Wanawake

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’