Kikosi cha Yanga kimetua mkoani Mbeya leo kwa usafiri wa Ndege na jioni kimefanya mazoezi tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya Vodacom dhidi ya Mbeya City.
Mchezo huo utapigwa kwenye dimba la Sokoine kesho Jumapili April 22 2018.

Yanga inahitaji kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo ili kurejesha matumaini ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo.
Matokeo ya sare ya bao 1-1 iliyopata Simba dhidi ya Lipuli yameirejesha Yanga kwenye mbio za ubingwa kwani kama itashinda michezo yake yote mitatu ya kiporo timu hizo zitatofautiana kwa alama tatu pekee na hivyo kuufanya mchezo baina yao uwe wa lazima kushinda April 29.

ADVERTISE HERE