Mahakama yatupilia mbali rufaa ya Magoma na wenzake

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Sep 2024
Mahakama yatupilia mbali rufaa ya Magoma na wenzake

Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam imetupilia mbali rufaa ya Juma Ally Magoma na mwenzake Geofrey Mwaipopo waliyokuwa wameikata dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Klabu ya Dar es Salaam, Young African Sports

Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu, Septemba 9, 2024 na Naibu wa Mahakama hiyo, Livini Lyakinana kwa niaba ya Jaji Mfawidhi, Salma Maghimbi aliyeisikiliza rufaa hiyo

Magoma na Mwaipopo walikata rufaa hiyo mahakamani hapo wakipinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dar es Salaam, Kisutu kuiongezea Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga na wenzake muda wa kufungua shauri la maombi ya marejeo

Yanga iliomba kuongezewa muda huo ili kufungua shauri hilo la marejeo ya hukumu ya mahakama hiyo iliyobatilisha Katiba yake ya sasa kufuatia kesi ya msingi iliyofunguliwa na Magoma na mwenzake, wakihoji uhalali wa katiba hiyo

Wajibu rufaa katika rufaa hiyo walikuwa ni Bodi ya Wadhamini ya Klabu ya Yanga (mjibu rufaa wa kwanza), Fatma Abeid Karume (mjumbe wa bodi hiyo mpaka sasa), Abeid Abeid na Jabiri Katundu, ambao pia waliwahi kuwa wajumbe wa bodi ya klabu hiyo

Bodi ya wadhamini wa Yanga imewawekea pingamizi la hoja za kisheria kina Magoma dhidi ya rufaa hiyo, ikibainisha hoja mbili

Kwanza inadai kuwa uamuzi ambao kina Magoma wameukatia rufaa na ya pili wanadai kuwa rufaa hiyo imeshapitwa na tukio

Pingamizi hilo lilisikilizwa Agosti 30 mwaka huu, ambapo mawakili pande zote Kalaghe Rashid wa Yanga na Jacob Mashenene wa kina Magoma walichuana kwa hoja za kisheria kila mmoja akijitahidi kuishaiwishi mahakama ikubaliane nao na kurejea kesi mbalimbali kusisitiza hoja zao

Hata hivyo Mahakama katika uamuzi wake imetupilia mbali rufaa hiyo baada ya kukubaliana na pingamizi la Yanga kuwa uamuzi waliokuwa wanaukatia rufaa haukupaswa kukatiwa rufaa kwa mujibu wa Sheria.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
25m ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
5h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
18h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
23h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’