Sakata la Kagoma lisitutoe kwenye reli - Manara

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Sep 2024
Sakata la Kagoma lisitutoe kwenye reli - Manara

Afisa Habari wa zamani wa Yanga Haji Manara amesema ni vyema sakata la usajili wa mchezaji Yusuph Kagoma likaachiwa Kamati ya TFF na Yanga ikajikita zaidi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CBE SA ambao utapigwa kesho Jumamosi huko Ethiopia

Baada ya taarifa iliyotolewa hapo jana na Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick kuhusu sakata la usajili wa mchezaji huyo, kumekuwa mijadala na majibizano baina ya maafisa wa Yanga, Fountain Gate na hata Simba

Manara amesema mijadala hiyo sio wakati wake kwani Yanga inapaswa kuweka nguvu katika mechi iliyo mbele ili kuhakikisha wanatinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa

"Na mimi nalisoma na kulisikia sakata la mchezaji Yussuf Kagoma kama tunavyosikia wengi. Ningeshauri jambo kwa Wanayanga wenzangu, hebu tufocus na mechi ngumu ya kesho ugenini dhidi ya Wahabesh"

"Wachezaji wetu wanasoma mitandaoni mabishano yetu na watani zetu na wao kama binadaamu wanaingia katika mkumbo wa kipi kiko focus zaidi"

"Tuitumie siku ya leo na kesho kuwaombea Mungu wafanye vizuri, tuwaonyeshe hili la kesho ni muhimu zaidi kwetu kuliko kuhangaika na jambo ambalo TFF bado hawajafanya maamuzi"

"Let's focus na vitu serious zaidi,hilo lingine tuliweke kiporo kwanza, tuwaambie wachezaji wetu tunahitaji kufuzu Group Stage kuliko kitu chochote kile kwa hivi sasa,tuwape nguvu na tuwaonyeshe kwamba tunawaamini na tunawategemea wao pale Addis Ababa hiyo kesho"

"Hamasa yetu huku na mitaani wanaisikia na kuiona na always huwapa nguvu kubwa ya kupambana zaidi," aliandika Manara katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
Magazeti ya leo Ijumaa, Oktoba 30 2026
1h ago
READ MORE β†’
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
13h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
17h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
22h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1d ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’