Yanga kutua Zanzibar Alhamisi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Sep 2024
Yanga kutua Zanzibar Alhamisi

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe ametangaza ratiba ya mabingwa hao wa nchi kuelekea mchezo wa mkondo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya CBE SA

Mchezo huo utapigwa Jumamosi, Septemba 21 katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, saa 2:30 usiku

Kamwe amesema baada ya timu kurejea kutoka Ethiopia, wameanza maandalizi kuelekea mchezo huo, kikosi kikitarajiwa kuelekea Zanzibar siku ya Alhamisi asubuhi

"Tayari tumeanza maandalizi yetu kuelekea mchezo dhidi ya CBE SA ambao utapigwa uwanja wa New Amaan Complex. Timu itaelekea Zanzibar siku ya Alhamisi, tutaondoka Dar es salaam na boti ya saa 3 asubuhi"

"Tutakuwa na siku mbili za kufanya mazoezi hapa Zanzibar kabla ya Jumamosi ambayo ni siku ya mchezo"

"Siku ya Ijumaa tutafanya dua maalum hapa Zanzibar kuiombea timu yetu, viongozi na mashabiki pamoja na kuwaombea ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki"

"Tayari mauzo ya tiketi kuelekea mchezo huo yameanza, tunawaomba mashabiki wetu hapa Zanzibar na wale watakaosafiri kutoka mikoa mbalimbali kununua tiketi zao mapema," alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
5h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
9h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
13h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’