Yanga imetinga hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa kibabe kwa ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya CBE katika mchezo uliopigwa uwanja wa New Amaan Complex
Ni ushindi wa jumla wa mabao 7-0 ikiwa ni pamoja na ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa mkondo wa kwanza
Clatous Chama ndiye aliyefungua ukurasa wa mabao akifunga bao maridadi la uongozi katika dakika ya 35 baada ya pasi ya Mudathir Yahya aliyekuwa kwenye kiwango bora
Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0 lakini mkeka wa mabao matano ukafuatia katika kipindi cha pili
Clement Mzize, Mudathir Yahya, Duke Abuya na Stephane Aziz Ki akifunga mabao mawili na kuihakikishia Yanga ushindi huo
Milioni 30 za Mama zimesoma katika akaunti ya Wananchi siku ya leo
Hongera Yanga kwa kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo