Chadrack Boka ameendelea kuwashangaza wengi kwa aina yake ya uchezaji, pengine ndiye mchezaji anayewapa furaha zaidi Wananchi
Kuna utani kuwa huyu Boka hapaswi kutumika katika viwanja vidogo kwani havimtoshi!
Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi analazimika kubadili mbinu zake pale anapocheza katika viwanja vidogo ili kuhakikisha Boka anaweza kutumika
Huu ni utani ulianzishwa na Wananchi lakini una ukweli ndani yake. Jana katika mchezo dhidi ya CBE Gamondi aliamua kumtumia Jonas Mkude eneo la Khalid Aucho na kazi ya Mkude ilikuwa kupiga pasi nyuma ya walinzi wa CBE na kumpa Bok nafasi ya kukimbia
Katika mabao sita ambayo Yanga walifunga kwenye mchezo huo, Boka alichangia mabao mawili na pengine ingekuwa zaidi
Kasi yake inamfanya kuwa mchezaji hatari sana hasa anapopata nafasi ya kukimbia. Ni ngumu kujua nafasi anayocheza ni beki au winga?
Yanga imewahi kuwa wachezaji wapima umri wa mabeki akina Tuisila Kisinda lakini huyu Boka sio kupima umri tu, anaweza kusababisha maafa!
Kwani ili kukimbizana nae pengine mabeki wa timu pinzani watalazimika kucheza na bodaboda kwa ajili ya tahadhari...!