Hatutawadharau Ken Gold - Kamwe

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Sep 2024
Hatutawadharau Ken Gold - Kamwe

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema wako mkoani Mbeya kwa kazi moja tu, kuhakikisha wanavuna alama zote tatu mkakati ukiwa kushinda mechi zote za viporo ili kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi

Kesho Jumatano Yanga watakuwa wageni wa Ken Gold katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine, saa 10 jioni

Licha ya Ken Gold kuburuza mkia katika msimamo wa ligi wakiwa wamepoteza mechi zote nne walizocheza mpaka sasa, Kamwe amesema timu hiyo sio dhaifu kama inavyoonekana na hawatawadharau

"Sisi tuko hapa kwa lengo moja tu, kusaka ushindi ili tuhakikishe tunakwenda pale juu kwenye msimamo wa ligi"

"Unajua kwa sasa ni ngumu kumueleza mtu ambaye yuko nje ya Tanzania kuwa ligi inaendelea hapa kwa sababu Yanga haipo kileleni. Hao wanaoshikilia nafasi ya kwanza hawafahamiki popote na hata wao wanajua wamekaa sehemu ambayo sio yao"

"Tunataka kushinda mechi zetu ili tuhakikishe tunakwenda kukaa katika nafasi yetu, msimu huu pia tumeweka malengo ya kushangilia ubingwa wa ligi kuu kwa mara ya nne mfululizo"

"Ken Gold tumeona mechi zao sio timu dhaifu, ila unaweza kusema walikosa bahati katika baadhi ya mechi ambazo walipoteza hivyo sisi hatuwadharau," alisema Kamwe

Kikosi cha Yanga kilitua mkoani Mbeya jana na leo jioni watafanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Sokoine

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’