Matchday: Ken Gold vs Yanga, NBC PL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Sep 2024
Matchday: Ken Gold vs Yanga, NBC PL

Mabingwa wa liigi kuu ya Tanzania Bara kwa misimu mitatu mfululizo Yanga leo wanarejea katika mikiki mikiki ya ligi baada ya kutimiza majukumu ya Kimataifa kwa kufuzu hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Yanga iko mkoani Mbeya kuikabili Ken Gold katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Sokoine, saa 10 jioni

Huu utakuwa mchezo wa pili wa ligi kwa Yanga msimu huu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa kwanza

Ni mchezo utakaozikutanisha timu mbili zenye malengo tofauti. Yanga inasaka ushindi ili kusogea juu katika msimamo wa ligi wakati Ken Gold bado wanasaka ushindi wao wa kwanza msimu huu

Ken Gold wako chini kabisa ya msimamo wa ligi wakipoteza mechi zote nne walizocheza. Pengine leo watajaribu kuzinduka mbele ya mabingwa watetezi

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi jana alisema hawaidharau Ken Gold kwani anatambua kila timu inayocheza na Yanga hupambana zaidi kusaka matokeo mazuri

Alisema hata kama Ken Gold walipoteza mechi zote zilizopita, mechi dhidi ya Yanga watakuwa tofauti na hivyo wachezaji wake ni lazima wapambane ili kushinda mchezo huo

Yanga ilitua Mbeya juzi na jana wakapata nafasi ya kufanya mazoezi ya mwisho katika uwanja wa Sokoine ambao mchezo huo utapigwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’