Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga watakuwa na jambo la katika uwanja wa Azam Complex
Ni saa 3 usiku Yanga itawakaribisha KMC ukiwa ni mchezo wa kwanza nyumbani kwa Yanga msimu huu
Jumapili ya kufosi, ndio kaulimbiu ambayo Wananchi wameamua kwenda nayo katika mchezo huo
Ni mchezo utakaozikutanisha timu zenye malengo tofauti. Yanga inasaka ushindi wa tatu mfululizo ili isogee juu zaidi katika msimamo wa ligi huku KMC wakisaka ushindi wao wa pili katika mechi ya sita msimu huu
Yanga imedhamiria kuendeleza umwamba dhidi ya watoza ushuru hao wa Manispaa ya Kinondoni, wakiwa na kumbukumbu ya kushinda mabao 5-0 msimu uliopita timu hizo zilipokutana Azam Complex
Yanga inakwenda kwenye mchezo huo ikiwa na kikosi chake kamili baada ya nahodha Bakari Mwamnyeto aliyekosa mechi mbili zilizopita akirejea baada ya kumaliza changamoto za kifamilia
Katika Mkutano na wanahabari jana, Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Miguel Gamondi alisema kimbinu mchezo huo utawapa burudani mashabiki kwani zinakutana timu mbili zinazopenda kucheza mpira
AIdha Gamondi alisisitiza kuwa wanachohitaji ni alama tatu bila ya kujali watafunga mabao mangapi katika mchezo huo