Mayele alipakumbuka nyumbani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
30 Sep 2024
Mayele alipakumbuka nyumbani

Jana Fiston Mayele alikuwepo uwanja wa Azam Complex, Chamazi kushuhudia mchezo wa ligi kuu kati ya Yanga dhidi ya KMC

Mayele alikaa jukwaani pamoja na Rais wa Yanga Injinia Hersi Said kushuhudia mchezo huo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0

Ujio wa Mayele unadhihirisha yake yaliyojitokeza mwanzo yamemalizika na kijana 'kiroho safi' ameamua kurejea nyumbani kusalimia

Jitihada kubwa zilifanyika kwa kuanzisha mgogoro uliokuwa na lengo la kumtenganisha Yanga na Mayele

Lakini ukweli ni kuwa Yanga imechangia kwa kiasi kikubwa kumfikisha Mayele hapo alipo lakini pia nae amekuwa na mchango mkubwa katika mafanikio ya Yanga hasa katika msimu wa 2022/23 ambao Yanga ilicheza fainali ya kombe la Shirikisho la CAF (CAF CC)

Mayele amesema yeye Yanga ni kama nyumbani na anajisikia faraja kuonana tena na wachezaji na viongozi aliofanya nao kazi kwa mafanikio makubwa

Aidha Mayele alimpongeza kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki kwa kuibuka MVP na mfungaji bora wa ligi kuu ya NBC msimu uliopita akimtaka kurudia mafanikio hayo msimu huu

"Nampongeza sana Aziz Ki kwa kuwa mfungaji bora msimu uliopita, ni ngumu kwa namba kumi lakini yeye ameweza, msimu huu nao pia akiendelea, apambane atafanya vizuri tu"

Mayele ambaye alipewa zawadi ya jezi na Aziz Ki mara baada ya wawili hao kukutana, amesema alipotua Tanzania siku moja kabla ya mechi hiyo akitokea Hispania kwa mapumziko, alifanya mawasiliano na fundi huyo wa Burkinafso ambaye alimsaidia kuwa mfungaji bora katika msimu wake wa mwisho akiwa na Wananchi na kumweleza atakuwa Chamazi katika mchezo huo wa ligi.

"Nilivyomweleza alifurahi na kusema atanipa zawadi ya bao na jezi. Hakufunga, lakini jambo muhimu nimeona alivyokuwa msaada kwa timu," ameongeza.

Mayele ambaye kwa sasa yupo nchini kwa mapunziko baada ya kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu Misri akiwa na Pyramids, alionekana akiingia uwanjani dakika chache kabla ya mchezo kuanza na wakati akiingia mashabiki wa Yanga walimpokea vizuri huku wakimpigia makofi.

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’