Lema anaitaka Ngao ya Jamii

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 Oct 2024
Lema anaitaka Ngao ya Jamii

Kocha Mkuu wa Yanga Princess Edna Lema amesema hawana hofu yoyote kuelekea mchezo wa nusu fainali Ngao ya Jamii dhidi ya Simba Queens utakaopigwa kesho Jumatano katika uwanja wa KMC

Akizungumza na Waandishi wa habari kuelekea mchezo huo mapema leo, Lema alisema wanawaheshimu Simba Queens kwa kuwa wana tmu nzuri iliyokuwa pamoja kwa muda mrefu lakini hawawaogopi

Lema amesema kikosi chake kimekuwa na maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo wakiwa na lengo la kushinda ili kutinga fainali na kutwaa Ngao ya Jamii

"Kama timu tumejiandaa vizuri, naamini utakuwa mchezo mgumu kwa timu zote kwani inakutanisha timu kubwa. Nawaheshimu Simba ni timu nzuri lakini hatuhofii kwani nasi tuna timu mpya ambayo imesheheni wachezaji wazuri sana"

"Matumaini ya kubeba ubingwa wa Ngao ya Jamii ni makubwa kwetu. Tukibeba ubingwa huu itatupa taswira ya kuanza msimu vizuri. Matarajio yetu mwaka huu ni kuwa mabingwa, unapopata mchezo mgumu kama huu unakujenga na kukupa majibu sahihi ya uimara wa timu yako”

"Tumeongeza wachezaji wengi wakigeni ambao ni wazuri sana. Lengo letu ni kuongeza ushindani ndani ya kikosi na upinzani wa kutosha dhidi ya washindani wetu. Naamini vijana hawa wapya watatupa ladha tofauti kuelekea mchezo wetu wa Derby"

"Wachezaji wangu hawana hofu, sisi hatuna hofu, uwezo wa kuonesha ubora wetu tunao. Tunaheshimu wapinzani wote ambao wapo kwenye mashindano haya ya ngao ya jamii. Binafsi niwe muwazi nilikuwa naitaka hii mechi ya Simba ili kupima ubora wangu. Ukitaka kujua ubora wako unapaswa kucheza na timu kubwa ili ujue uimara na mapungufu yako," alisema Lema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’