Yanga Princess leo imemaliza unyonge dhidi ya watani zao Simba Queens wakitinga fainali ya Ngao ya Jamii kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 baada ya matokeo ya sare ya bao 1-1
Ni wazi msimu huu Yanga Princess inakwenda kushindana, leo kocha Edna Lema na vijana wake wamedhihirisha sasa wako tayari kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Wanawake
Alikuwa ni Agnes Pallangyo aliyeitanguliza Yanga Princess kwa bao la mapema dakika ya kwanza bao lililodumu kwa dakika 90 kabla ya Simba Queens kusawazisha dakika za lala salama
Lakini mikwaju ya penati ikaamua ushindi kwa Yanga Princess ambayo leo ilistahili kushinda
Mlinda lango wa Yanga Princess Rita Akarekor aliibuka shujaa akiokoa mikwaju mitatu ya penati
Yanga Princess sasa watachuana na JKT Queens katika mchezo wa fainali
Lema amedhihirisha yeye ni kiboko ya Simba Queens kwani kabla ya mchezo wa leo, mechi yake ya mwisho dhidi ya Simba Queens aliongoza Yanga Princess kupata ushindi wa bao 1-0